Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MKEMIA MKUU AWATAKA MADEREVA KUTUMIA ELIMU KUEPUSHA AJALI ZA KEMIKALI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka madereva wanaosafirisha mizigo ya kemikali kutumia elimu waliyopata katika kuepusha ajali za kemikali ili kulinda afya za binadamu na mazingira.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya usafirishaji salama wa kemikali kwa madereva 36 kutoka kampuni zinazojihusisha na usafirishaji wa mizigo ya kemikali, Mkemia Mkuu wa Serikali amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu juu ya usafirishaji salama wa kemikali na misingi ya kufahamu kemikali ni hatari hivyo wanaposafirisha mizigo hiyo wanapaswa kuwa makini ili kulinda afya ya dereva mwenyewe, wananchi na mazingira anayopita.

“Napenda kuwapongeza sana kwa kuhudhuria mafunzo haya na kupata elimu kuhusiana na usafirishaji salama wa kemikali. Mnapaswa kufahamu lengo la mafunzo haya ni kuwapatia ufahamu juu ya usafirishaji salama wa mizigo ya kemikali kwa lengo la kulinda afya zenu, wananchi na mazingira mnayopita wakati wa kusafirisha kemikali. Nimefurahi kusikia kwa kauli zenu kama madereva kwamba mafunzo haya yamewabadilisha na kuwafanya kuwa madereva bora na makini zaidi, kwa sababu lengo la mafunzo pia ilikuwa ni kuwapatia uelewa kuhusu namna bora na salama ya usafirishaji wa kemikali na kwa kauli zenu wenyewe kuniambia kwamba mafunzo haya yamewabadilisha basi kwangu ni faraja kubwa kwani inanipa moyo wa matumaini na kunithibitishia kuwa timu iliyotoa mafunzo haya imefanikiwa kutimiza lengo.”

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali aliwataka kutambua vyeti walivyopewa sio tu alama au pambo la kumaanisha wamemaliza mafunzo bali wakatumie elimu waliyopata kuwaelimisha madereva wengine ambao hawajafanikiwa kupata mafunzo kwa lengo la kuepusha ajali za kemikali na kulinda afya ya binadamu na mazingira.

“Vyeti mlivyopewa leo isiwe ni kama pambo au sifa tu ya kuonesha umepitia mafunzo kuhusu usafirishaji salama wa kemikali bali mnapaswa kuvitumia pamoja na elimu mliyopatiwa kusaidia kuepusha ajali za kemikali ikiwemo kuwaelimisha madereva wenzenu ambao hawajafanikiwa kupata mafunzo ili kulinda afya za binadamu na mazingira. Katika masuala ya maslahi yenu tutajitahidi kujenga ushawishi kwa ngazi nyingine zinazohusika pale tunapopata nafasi ili kuweza kufikisha kilio chenu.” Alimaliza.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya madereva wenzake walioshiriki mafunzo hayo, Theobald Batholomeo Makanji, alisema mafunzo waliyopata ndani ya siku mbili hawakuyategemea na yamewabadilisha kiuwezo na wanajiona ni madereva wapya watakaofanyakazi kwa ufanisi mkubwa.

“Kwa niaba ya madereva wenzangu tunashukuru kwa mafunzo mazuri maana yametubadilisha na kutufanya kuwa madereva wapya. Sasa tunaelewa namna ya usafirishaji salama wa kemikali kuanzia kwenye maandalizi ya mzigo kupakia, kusafirisha na mpaka kushusha. Kemikali ni muhimu na ni hatari hivyo usafirishaji wake unapaswa kuwa na umakini ili ifike salama. Tumepata mafunzo katika hali ya weledi mkubwa na tumependa na tunaahidi kuwa mabalozi wazuri barabarani.” 

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.