Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YAFANYA MNADA WA KEMIKALI

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, leo tarehe 27 Julai, 2019, imeuza kwa mnada wa hadhara kemikali aina ya “Portable Extra Neutral Alcohol” iliyokuwa kwenye jumla ya mapipa 160 (mia moja sitini) (yenye ujazo wa lita 250 (mia mbili na hamsini ) kila moja.

Akiongea wakati wa mnada huo, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kemikali,Bw. Daniel Ndiyo alieleza kuwa, Mamlaka imeuza kemikali hizo baada ya kuingizwa nchini kinyume cha Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Na. 3 ya Mwaka 2003 mnamo mwezi Disemba 2017. Mkurugenzi Ndiyo aliendelea kuweka bayana kuwa, kutokana na ukiukwaji huo wa Sheria,  hatua za kisheria zilichukuliwa kwa mhusika kufikishwa mahakamani na baada ya kukutwa na hatia,  Mahakama iliagiza kemikali hizo zitaifishwe na Serikali na kuuzwa kwa njia ya mnada. 

“Baadhi ya taratibu zinazotakiwa kufuatwa ni pamoja na kufanya usajili kwa kila mdau anayejishughulisha na biashara ya kemikali, na kuomba na kupata kibali cha kuingiza nchini kila aina ya kemikali inayoingizwa. Hata hivyo, taratibu hizo hazikufuatwa na mhusika wa kemikali hizo zilizopigwa mnada.”

Mnada huo uliongozwa na Bw. Ismael Ogaga, Mhakikimali wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Makao Makuu ambapo Kampuni ya EKMAJM Investment ilifanikiwa kununua kemikali hizo kwa gharama ya shilingi milioni mia moja na laki nane (TZS 1,800,000.00) baada ya kuyashinda makampuni mengine saba yaliyoshiriki.

Akiongea baada ya kushinda mnada huo, Mwakilishi wa kampuni hiyo Bwana Alfred Mtei alisema kuwa, wamefurahi kushinda na kununua kemikali hizo maana zitawasaidia katika shughuli za kibiashara kwa maana wamezipata kwa haraka kuliko wangeagiza ambapo zingechukua muda kufika. “ Sisi ni wafanyabiashara wa kemikali na huwa tunaagiza kutoka nje na kwa ajili ya kuja kuuza kwa wadau wengine. Tumefurahi kushinda mnada huu kwa sababu imetusaidia kuokoa muda ambao tungetumia kuagiza kutoka nje lakini tumezipata hapa na kwenda kuendelea na biashara moja kwa moja.”

Makampuni mengine ambayo yalishiriki mnada huo ni Mega Beverages Ltd, Sakwa foods, Semtema Distillers Coy Ltd, Karantini Coy Ltd, Okwood Holdings Ltd, Profil Eeda Masawe na A.A. Pharmaceutical Ltd

Katika mnada huo kemikali zote ziliuzwa katika kundi moja mapipa yote mia moja na sitini (160) na mnunuzi alifanikiwa kulipa malipo yote baada ya kukamilika kwa mnada. 

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.