Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
RAIS, DKT. MAGUFULI: NAWAPONGEZA KWA NIABA YA TAIFA MMEFANYA KAZI KUBWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapongeza watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi kubwa ya uchunguzi na utambuzi wa miili ya marehemu hamsini kati ya sitini na tisa waliofariki katika ajali ya moto iliyotokana na kulipuka kwa gari lililokuwa limebeba petroli iliyotokea tarehe 10 Agosti, 2019 mkoani Morogoro.

Mhe. Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo alipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa lengo la kutembelea maabara ya uchunguzi wa vinasaba na kuongea na watumishi wa Mamlaka, Makao Makuu.

“Nawapongeza na kuwashukuru kwa niaba ya watanzania kwa kazi kubwa mliyoifanya ya kuweza kufanya uchunguzi na kutambua miili ya marehemu hamsini kati ya sitini na tisa waliofariki katika ajali ya moto Morogoro. Kazi mliyofanya si ndogo kufanywa na Taifa kama Tanzania na kusimamiwa na watanzania wenyewe, niwahakikishie kazi mnayofanya inathaminika sana na Serikali.  Natambua hamkulala toka ilipotokea ajali na mlichukua sampuli za marehemu wote usiku kucha na sasa baada ya ripoti hii itasomwa ili ndugu wasikie na kutambua ndugu zao waliozikwa kwa kutumia namba kule Morogoro.

Rais Dkt. John Magufuli amesema tusiwalaumu marehemu bali tujiweke kwenye nafasi yao ya kuona mafuta yanamwagika na unaweza kufanya kitu ili kuzuia upotevu huo na bila kutarajia ajali ya moto ikatokea.

“Tusiwalaumu marehemu ila tutimize wajibu wetu wa kuwaombea nasi tukijiombea na vyombo vya ulinzi kuendelea kuchukua tahadhari kwa matukio yanayoweza kuhatarisha maisha ya yetu. Kwa hawa marehemu kumi na tisa ambao bado hawajatambulika inabidi taarifa kutangazwa ili ndugu zao wajitokeze. “

 “Kuhusu changamoto zenu nimewasikia inawezekana nisiwe na jibu leo, nimeona mnayofanya na hatari inayoendana na kazi zenu kama kuvuta hewa isiyo salama na matumizi ya kemikali. Nitakaa na wenzangu na kuona nini cha kufanya kwa sababu mnastahili zaidi, nimewaelewa.”

Niwaombe muendelee kutunza siri ya haya mnayoyafanya maana yanahatarisha maisha yenu, mjiepusha na tamaa na rushwa kwa sababu itagharimu maisha yenu.”

Aidha, Rais Magufuli amevitaka vyombo vya ulinzi na Usalama kulinda maisha ya watumishi wanaokwenda kutoa ushahidi wa kitaalam mahakamani unaohusiana na kesi za Jinai kama dawa za kulevya, ubakaji na mauaji.

“Vyombo vya ulinzi na usalama mnatakiwa kuangalia maisha ya watoa ushahidi mahakamani kwa kuangalia namna gani ya kuwalinda wanapokwenda kutoa ushahidi maana kesi nyingine kama za dawa za kulevya kunakuwa na watu wenye uwezo ambao wanaweza kuwadhuru au kuwafanya wasitoe ushahidi vizuri kwa kuhofia maisha yao. Kila mmoja wenu akatembee kifua mbele kwa hili mlilofanya na mnavyoendelea kuchapa kazi” Alimaliza.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.