Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
WADAU WATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI YA KEMIKALI BASHIRIFU

Wadau wanaoagiza, kusafirisha na kutumia kemikali bashirifu nchini wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya kemikali hizo ili kuepusha kuchepushwa na kutumika kinyume na matumizi yaliyolengwa ikiwemo kutengeneza dawa za kulevya.

Akiongea kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka za Udhibiti na wadau wa Sekta binafsi katika kuzuia uchepushaji wa kemikali bashirifu, Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias, alisema Serikali imekuwa ikitumia njia mbalimbali ili kuongeza jitihada ikiwemo kutunga Sheria kwa lengo la kupambana na kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu ambazo zinaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.

“Kama njia mojawapo ya kusimamia mwenendo wa biashara na matumizi ya kemikali bashirifu, Serikali kupitia Mamlaka za udhibiti imeunda Sheria na Kanuni mbalimbali za kusimamia na kudhibiti uingizaji, usambazaji, usafirishaji, utumiaji, utekelezaji na usafirishaji wa kemikali nje ya nchi. Hivyo, ni muhimu kwa wadau wa sekta binafsi wanaojishughulisha na kemikali mbalimbali ikiwa pamoja na kemikali bashirifu, kuelewa Sheria na kanuni ili kuzitekeleza.”

Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, alisema mkutano huo utatoa ufafanuzi juu ya uchepushaji wa kemikali bashirifu na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika udhibiti.

“Ni matumaini yetu kwamba wadau mliopo kwenye mkutano huu mtapata uelewa wa kemikali bashirifu ni nini na umuhimu wa kudhibiti, uelewa wa Sheria na kanuni za udhibiti na mbinu zinazotumika katika kuchepusha kemikali hizo, hivyo naomba muwe huru kujadiliana, kutoa mapendekezo ya namna bora ya kushirikiana kati ya Mamlaka za Udhibiti na Sekta binafsi ili kufikia lengo la Serikali katika kudhibiti mianya yote inayoruhusu uchepushwaji wa kemikali bashirifu” alimaliza.

Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai kutoka Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Bertha Mamuya, akiongea kwa niaba ya Kamishna Jenerali, alisema wanaamini ushirikishwaji wa wadau wa kemikali utaongeza ufanisi katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali.

“Kama Serikali tunaamini ushirikiano na wadau wa kemikali katika kujisimamia na kushirikiana na Mamlaka husika kutaongeza ufanisi katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu hivyo kufanikisha vita dhidi ya dawa za kulevya. Ni matumaini yangu majadiliano katika mkutano huu yatachagiza nia njema ya uanzishwaji wa ushirikiano wa hiari kati ya wadau na Mamlaka za udhibiti ili kufanikisha lengo la Serikali katika upatikanaji wa dawa za kulevya.”

Mamlaka za udhibiti zilizoshiriki katika mkutano huo ni Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Baraza la Famasia Tanzania, Bohari ya Dawa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba na kuhusisha wadau mia moja wanaojihusisha na shughuli kemikali na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam.

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.