Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MAMLAKA YATOA MAFUNZO KWA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason amewataka wahariri wa vyombo vya habari kuyafahamu majukumu ya Mamlaka ili kuweza kusaidia kuelimisha umma kwa usahihi wanapoandika habari zinazohusiana na utendaji wa Mamlaka.

Mwenyekiti wa Bodi ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wahariri na waandishi wa habari yaliyoandaliwa na Mamlaka kwa lengo la kuwaelimisha majukumu ya Mamlaka kwa Serikali na Umma wa Watanzania.

“Majukumu ya Mamlaka yamegawanyika katika maeneo makuu matatu ambayo ni Uchunguzi wa Kimaabara wa Sampuli na Vielelezo mbalimbali; Utekelezaji wa Sheria tatu ambazo Mamlaka inasimamia na kutoa ushahidi wa kitalaamu kwenye masuala yanayohusu uchunguzi wa kimaabara katika  mahakama mbalimbali nchini.

Kuna majukumu mengine mengi ambayo Mamlaka inatekeleza na yanapaswa kufahamika moja kwa moja na jamii. Ikiwa ni sehemu ya kujenga uelewa wa majukumu yake,  Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeandaa mafunzo haya kwenu ninyi Wahariri wa Vyombo vya Habari ili muweze kuelewa majukumu mahususi ya Mamlaka hii. Pia, kupitia mafunzo haya mtaweza kufahamu majukumu yapi ni kwa ajili ya umma kufahamu moja kwa moja na ni yapi kwa ajili kuwezesha utoaji wa maamuzi katika mashauri mbalimbali mahakamani.

Mtaweza kupata elimu ya majukumu ya Mamlaka katika ujumla wake na majukumu kutoka kila Idara zinazounda Mamlaka hii. Wito wangu kwenu ni kuwaomba kuwa washiriki wema na kuweza kupata nafasi ya kubadilishana mawazo na wawezeshaji ili kupata uelewa unaojitosheleza na hatimaye kuwa mabalozi wema na wenye taarifa sahihi. Ni matarajio yangu kuwa, kupitia ninyi na elimu mtakayoipata, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali itatambulika na kufahamika kwa usahihi zaidi kwa kuzingatia majukumu inayotekeleza” alimalizia.

Akiongea kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, aliwashukuru wahariri kwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo na anaamini kwa kutumia taaluma yao watasaidia kuandika na kuelimisha umma kikamilifu.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wahariri hamsini na sita kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya umma na binafsi.   

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.