Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
DKT. NDUGULILE: GCLA NI TAASISI YA KIMKAKATI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni taasisi ni moja ya taasisi ya kimkakati katika taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya.

 Akiongea na Watumishi baada ya kutembelea maabara, Naibu Waziri, Dkt. Ndugulile, alisema Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni taasisi ya kimkakati na muhimu kwenye masuala ya kiuchunguzi wa maabara kwa sababu inajihusisha na uchunguzi wa sumu, vinasaba, kemikali na dawa za kulevya.

“Tunawekeza na kuiboresha taasisi hii ili iwe ya kisasa zaidi na tutaendelea kuwekeza ili kuimarisha utendaji wake ili umuhimu na ubora wa huduma tunazotoa zisiwe na mashaka.  Maabara zina utaratibu wake kuanzia sampuli inapopokelewa mpaka inapotoka, mnyororo mzima lazima uwe vizuri ili kila kitu kiwe kimekaa kwenye utaratibu wake.”

Naibu Waziri aliagiza Menejimenti kuharakisha mchakato wa kuzipatia ithibati maabara ambazo bado hazijapata ili kuzipa nguvu zaidi ya kiuchunguzi katika ngazi ya kimataifa na pia kuwasifu watumishi wa Mamlaka kwa kufanyakazi nzuri kwa kuzingatia maadili na taaluma.

“Hakikisheni maabara zilizobaki zinapata ithibati ili kuzipa nguvu kimataifa ingawa mnafanya mitihani ya kujipima ya kimataifa kwa sasa. Mmejijengea heshima na mnafanyakazi nzuri kwa kuzingatia maadili na taaluma, mimi na Waziri wa Afya tunajisifia sana taasisi hii na tutaendelea kuwapa ushirikiano”

Akitoa neno la shukrani, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, alisema anamshukuru Naibu Waziri kutembelea Mamlaka na maelekezo aliyoyatoa yatafanyiwa kazi ndani ya siku saba.

“Maelekezo yako Mheshimiwa Naibu Waziri yamekuwa yakitaalam na tumeyapokea na tunaahidi kuyatekeleza. Umetuasa maadili na kuzingatia miiko ya taaluma zetu, tunakuahidi tutaendelea kuzingatia na kukumbusha katika hayo”alimaliza.

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.