Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MAMLAKA YAELEZA MAFANIKIO YA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amezungumzia mafanikio ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Akiongea katika Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Mkemia Mkuu wa Serikali, alielezea mafanikio katika maeneo makubwa kumi na mbili (12) ambayo ni;

1.    Uwekezaji katika Miundombinu ya Maabara za uchunguzi ambapo alielezea katika eneo la vifaa kwa maana ya mitambo ya kisasa,mifumo ya TEHAMA pamoja na majengo ambapo kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 6.5 zimetumika katika uwekezaji huo ndani ya kipindi cha miaka minne.

2.    Ongezeko la Rasilimali Watu/Wataalam ambapo idadi imeongezeka kutoka watumishi 203 na kufikia 293 na kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku kama ukaguzi wa kemikali, uchunguzi wa kimaabara na utoaji ushahidi mahakamani ili kusaidia vyombo vingine kutenda haki.

3.    Kuimarisha usimamizi na udhibiti wa Kemikali kwa lengo la kulinda Afya za Wananchi na Mazingira dhidi ya matumizi yasiyo salama ya kemikali ambapo imepelekea wadau wengi wa kemikali kusajili, kuwa na ukaguzi wa masaa 24 kwa siku 7 kwa maeneo ya mipakani na kuimarisha usimamizi na udhibiti wa kemikali na kemikali taka hatarishi kwa kuweka utaratibu wa kusindikiza usafirishaji wa baadhi ya kemikali hatarishi kama “ammonium nitrate na sodium cyanide.” Kwa lengo la kuwezesha kasi ya ukuaji wa Viwanda.

4.    Kuwezesha na kuchangia juhudi za Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda ambapo Mamlaka kupitia Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango imefuta jumla ya tozo 17, na kupunguza tozo 8 katika utekelezaji wa Sheria ya Kemikali. Hali hii imewezesha kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania kwa kupunguza mzigo wa gharama kwa wafanya biashara wa kemikali katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Pia, kufanya marekebisho ya Sheria ya Kemikali za Viwandani na Majumbani Namba 3 ya Mwaka 2003 kwa kufanya maboresho ya kifungu cha 43(11) ili kuruhusu uingizaji wa kemikali katika ujazo mkubwa usiokuwa kwenye vifungashio (bulk).

5.    Mafanikio katika uchunguzi wa kimaabara kutoka kuchunguza sampuli 34,937 mwaka 2015/2016 mpaka sampuli 82,508 kwa mwaka 2018/2019.

6.    Kuhuisha mifumo ya ithibati na katika kipindi cha Miaka minne Mamlaka imefanikiwa kuhuisha mfumo wa ithibati ya menejimenti kutoka ISO 9001: 2008 kwenda ISO 9001:2015 mwaka 2019. Vile vile, Mamlaka imehuisha ithibati ya Maabara ya chakula kutoka ISO 17025:2005 kwenda ISO 17025:2017. Mifumo hii inasaidia kuboresha mifumo ya utendaji na kuboresha utoaji wa huduma bora kwa serikali na wadau mbalimbali wa shughuli za Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

7.    Ushiriki katika Majanga Makubwa na Uwezo wa Utambuzi wa miili iliyoharibika na iliweza kushiriki katika majanga ya Kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere – Ukerewe mwaka 2018, Ajali ya gari la abiria iliyotokea Tarime – Mara mwaka 2018, Ajali ya Tanki la Mafuta tarehe 10.08.2019 – Morogoro na Ajali ya Lori lililopata ajali na kuwaka moto Kibiti – Pwani mwaka 2019. Katika uchunguzi wa vinasaba uliweza kutambua Miili 88 katika jumla ya miili 98 iliyofanyiwa uchunguzi ilitambuliwa baada ya ulinganifu wa ndugu na jamaa na miili kumi ndugu hawajajitokeza kwa ajili ya kupata sampuli za kulinganisha.

8.    Kuimarika kwa Mafunzo na Elimu kwa Wadau wa Mamlaka na katika kipindi cha miaka minne jumla ya wadau 11, 598 wameweza kufikiwa kwa njia ya mafunzo kwa wadau, mfano, wanaojishughulisha na kemikali, Jeshi la polisi, madaktari, wanasheria, wachimbaji wa madini na kwa njia ya kujitangaza kupitia vyombo vya habari, ushiriki katika maonesho mbalimbali na makongamano kwa lengo la kuufahamisha umma majukumu ya Mamlaka.

9.    Kuimarisha Utaalam na uwezo wa Watumishi kupitia mafunzo ya muda mrefu na mfupi ikiwemo ushiriki wa majaribio ya umahiri katika uchunguzi wa maabara (Proficiency Test) kila mwaka. Ambapo matokeo ya majaribio kwa Mamlaka yamekuwa na mafanikio makubwa.

10. Kuongezeka kwa Mapato ya Mamlaka kutoka bilioni 9.342 mwaka 2015/2016 mpaka bilioni 24.246 mwaka 208/2019. Mapato hayo yameongezeka kutokana na kuimarishwa kwa mifumo ya udhibiti na ukusanyaji wa mapato (Epicor na GePG) na kuimarika kwa mifumo ya ndani ya ukaguzi na udhibiti fedha na utunzaji wa hesabu. Fedha hizi zimesaidia katika ununuzi na ukarabati wa mitambo ya maabara, kuboresha miundombinu ya maabara, kununua vitendanishi na kuimarisha Ukaguzi wa Kemikali.

 

11.  Kuchangia katika tiba kwa kutoa ushauri wa kitaalam kwa taasisi za tiba kwa kufanya uchunguzi wa kimaabara kwa kutumia teknolojia ya vinasaba vya binadamu kwenye uchunguzi wa kutambua uhusiano wa mtoaji na mpokeaji wa figo (kidney transplant) ili kuwezesha upandikizaji kwa mtu mwingine kwa mafanikio. Pia kufanya uchunguzi wa kuwezesha utambuzi wa jinsi tawala (sex identification) kwa watoto wanaozaliwa na jinsi mbili ili kuweza kupata matibabu stahiki kwa watu wanaozaliwa na jinsia mbili. Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kufanya uchunguzi wa ulinganishi kwa ajili ya upandikizaji wa figo kwa sampuli 29 na utambuzi wa jinsi tawala 48.

 

12. Ongezeko la Matumizi ya TEHAMA katika kutekeleza Majukumu ya Mamlaka ambapo imeweza kuanzisha mfumo wa Usajili wa Wadau wa Kemikali kwa njia ya Mtandao, kutumia mfumo mpya wa usimamizi wa fedha (Epicor Version 10), kutumia mfumo wa ukusanyi maduhuli na malipo ya Serikali (GePG) na kukaribia kukamilisha mfumo wa Menejimenti ya Nyaraka  (e-Office).

Akizungumzia mipango ya baadae ya Mamlaka, Mkemia Mkuu wa Serikali, alisema ni;

  1.  Kuendelea kuimarisha mahusiano na taasisi zinazotoa huduma za afya hasa katika matibabu ya kisasa yanayohusisha tiba ya "gene therapy", matibabu ya Figo, utambuzi wa jinsi tawala (Sex ambiguity).
  2. Uanzishwaji wa Kanzidata ya Taifa ya Vinasaba vya Binadamu
  3. Kuimarisha ofisi za Kanda kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
  4. Ujenzi wa miundombinu mingine ya TEHAMA.
Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.