Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUZINGATIA KUZINGATIA MATUMIZI SALAMA YA KEMIKALI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka wajasiriamali wanaotumia kemikali katika uzalishaji wa bidhaa kuzingatia usalama wa afya na mazingira wanayotumia kemikali hizo.

Mkema Mkuu wa Serikali ameyasema hayo leo Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wajasiriamali wadogo na wa kati wanaotumia kemikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki na kufanyika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam.

“Matumizi mabaya ya kemikali huweza kusababisha madhara kama magonjwa, mfano saratani, mfumo wa uzazi na urithi, mfumo wa upumuaji na hatimaye kifo. Pia, matumizi ya kemikali yasiyo sahihi ya kemikali huathiri mazingira kama maji, misitu na kudhuru wanyama pori, ngozi n.k. Ili kuepukana na haya madhara, matumizi salama ya kemikali ni suala la lazima kwa lengo la kulinda afya na mazingira.

Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepatiwa jukumu la kutoa elimu na mafunzo kuhusu Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali kwa wadau wanaojishugulisha na Kemikali. Aidha, Mamlaka inatoa elimu na semina kwa wadau wa makundi mbalimbali yanayojishughulisha na matumizi au biashara ya Kemikali mkiwemo ninyi wajasiriamali kwa lengo kuu la kuelimisha kila kundi liwe na uelewa wa kutosha kuhusu kemikali na kuzitumia bila kuleta madhara kwa afya na mazingira.

Ni matumaini yangu kuwa utoaji wa mafunzo na semina kama hizi utapelekea kuwa na idadi kubwa ya wadau  wengi wa shughuli za kemikali wenye weledi wa kusimamia vyema shughuli hizo na hivyo kuimarisha jitihada za utekelezaji wa sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani namba 3 ya mwaka 2003, na Kanuni zake za mwaka 2015” alisema.

Akiongea kwa niaba ya wajasiriamali waliohudhuria semina hiyo Mkufunzi wa Ujasiriamali kutoka Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO), George Buchafwe, aliishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki kwa kuandaa semina hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo na maarifa zaidi wajasiriamali wanaotumia kemikali katika kuzalisha bidhaa zao mbalimbali.

“Tunatunguliza shukrani zetu za dhati na tunawapongeza kwa kuandaa semina hii juu ya matumizi salama ya kemikali, tunaamini itatusaidia katika matumizi salama ya kemikali kwenye kazi zetu na kusaidia kulinda afya zetu na mazingira tunayotumia kuzalishia bidhaa zetu. Tunaahidi kuzingatia elimu tutakayoipata leo katika kuimarisha shughuli za utengenezaji wa bidhaa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali kama ilivyoeleza na Mkemia Mkuu wa Serikali leo.”

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.