Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
WADAU WAKUTANA KUJADILI KEMIKALI ZINAZOHARIBU TABAKA LA HEWA

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amezitaka taasisi za Udhibiti wa Kemikali na wadau kujadili namna bora ya kusimamia na kudhibiti kemikali zinazoharibu tabaka la hewa kulingana na makubaliano ya Protokali ya Montreal.

Mkemia Mkuu wa Serikali amesema hayo leo jiji Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha pamoja kati ya Mamlaka za Udhibiti wa Kemikali hizo na wadau kujadili namna ya kuimarisha udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la hewa.

“Naelewa majadiliano ya kikao hiki yanalenga kuweka utaratibu wa kuboresha utekelezaji wa Protokali ya Montreal ya mwaka 1987 ikizingatiwa kuwa kemikali chini ya Protokali hiyo zinatakiwa kufikia ukomo wa matumizi yake mwaka 2030.

Najua mtapata uelewa wa majukumu ya kila taasisi inayohusika na Protokali hiyo ndani ya serikali pamoja na wajibu wenu nyinyi kama wadau mnaojishughulisha na kemikali hizo. 

Pia katika kikao hiki mtajadili kwa pamoja namna ya kuanza kupunguza kiasi cha uingizaji wa kemikali hizo kufikia mwaka 2030 ambapo zitaondolewa kabisa katika matumizi na kusitishwa uzalishaji wake. Ni imani yangu mtajikita katika kuweka msisitizo wa kupunguza na kukomesha uagizaji wa kemikali hizi kwa lengo la kuweka mazingira ya nchi yetu salama dhidi ya uharibu wa tabaka la hewa la Ozone” alimaliza.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kemikali nchini, Daniel Ndiyo, akiongea baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali, alisema kikao hicho kimehusisha pia wadau kwa lengo la kujadili kwa pamoja na kukubaliana utaratibu utakaotumika ili kuimarisha utekelezaji wa protokali ya Montreal inayosimamia kemikali zinazoharibu tabaka la hewa.

“Mjadala wetu utajikita katika kutengeneza na kukubaliana utaratibu wa kupunguza uingizaji na utumiaji wa kemikali hizo ili ifikapo mwaka 2030, kemikali hizo ziwe zimeondolewa katika matumizi na mbadala wake ndio ziwe zinatumika” aliongeza.

Baadhi ya kemikali ambazo zinahusishwa na uharibifu wa tabaka la hewa ni kama chlorofluorocarbons (CFCs), hydro chlorofluorocarbons (HCFCs), halons, methyl bromide, carbon tetrachloride, hydrobromofluorocarbons, chlorobromomethane, and methyl chloroform ambazo hutumika kama gesi za kwenye magari, friji n.k.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.