Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MKEMIA MKUU WA SERIKALI AWATAKA WAKAGUZI KUBORESHA UTENDAJI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka wakaguzi wa kemikali

kwenda kutekeleza kwa kuzingatia maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusiana na changamoto za ujazaji wa fomu za maombi ya usajili wa wadau wa kemikali.

Mkemia Mkuu wa Serikali ameyasema hayo jana wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali uliofanyika katika Ukumbi wa NSSF, Ilala, Dar es Salaam.

“Mkatekeleze maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusu ujazaji wa fomu za taarifa za wadau wa kemikali, maoni na alama walizopata kwa ajili ya kukidhi vigezo vya kusajiliwa, zoezi hili linapaswa kuboreshwa kuanzia kwa mkaguzi, msimamizi na Mameneja wanaohusika na usajili. Ni eneo ambalo linahitaji kujengeana uwezo ili kuweza kuboresha zaidi na kutiliana mkazo, Bodi inapongeza kwa hatua tuliyofikia na mtazamo wa Bodi ni chanya, nanyi mnapaswa kupokea kwa mtazamo chanya kwa sababu lengo ni kuboresha utendaji wetu.

Changamoto za usafiri na makazi kwa wakaguzi wa mipakani zinaendelea kufanyiwa kazi na kwa kuanza ile mipaka ambayo ilionekana na changamoto ya usafiri imepatiwa pikipiki na changamoto nyingine zinaendelea kufanyiwa kazi kulingana na taratibu za Serikali. Tuache kufanyakazi kwa mazoea na kila mmoja ajue ana jukumu la kutimiza kama kuna changamoto wasiliana na kiongozi wako kupata ufumbuzi.”

Mkemia Mkuu wa Serikali aliwataka wakaguzi wa kemikali kuimarisha mahusiano na wadau wanapotekeleza majukumu yao ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma kwa wateja.

“Mnapaswa kuzingatia na kuimarisha mahusiano na wadau. Kutekeleza Sheria haimaanisha kutumia ubabe au lugha isiyo rafiki, tutekeleze Sheria lakini tutumie busara na akili za ziada ili kuwezesha kazi na kila mmoja ajiongeze na afanye inavyotakiwa” alisema.

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali amewaeleza Wakaguzi wa Kemikali kwenda kufanyia kazi yaliyojadiliwa ili mkutano wa mwakani uoneshe tija kwa yale yote ambayo wamekubaliana kwenda kuyatekeleza.

“Nawapongeza kwa mkutano wa mwaka huu kwa sababu umekuwa shirikishi na watu wameongea kwa lengo la kujenga. Natarajia mkutano ujao tukutane huku kila mkaguzi akionesha ametekeleza sehemu yake na hiyo itasaidia kuonesha mafanikio ya mkutano huu kutoka mwaka mmoja na mwingine” alimaliza.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakaguzi wa kemikali, Revocatus Mwamba, kutoka Ofisi ya Kanda ya Kati, alishukuru kwa ushirikiano unaotolewa na Menejimenti katika kuwezesha kutekeleza majukumu ya Mamlaka kwa ufanisi na aliomba ushirikiano huo uendelee kwa lengo la kutimiza matakwa ya Serikali na taasisi kwa ujumla.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.