Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MADEREVA 100 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA USAFIRISHAJI SALAMA KEMIKALI HATARISHI

Madereva zaidi ya 100 wanaojihusisha na usafirishaji wa Kemikali na Mizigo Mingine Hatarishi nchini wamenufaika na mafunzo ya Usafirishaji salama wa kemikali mbalimbali yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Kanda ya Mashariki, na kutajwa kuwa yatawasaidia kuzingatia kikamilifu sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na majumbani ya Mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2020.

Akifunga Mafunzo hayo Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali David Elias amewataka madereva wote waliopatiwa mafunzo hayo, kuzingatia kwa uhalisia yale yote waliojifunza kuhusiana na usafirishaji wa Kemikali ili kuweza kusafirisha salama kemikali hizo bila kujitokeza kwa madhara ya aina yoyote.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa siku mbili yamehusisha mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na taasisi nyingine za serikali ikiwemo mada ya sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za Viwandani na Majumbani ya Mwaka 2003.

Madereva wote walioshiriki kwenye mafunzo hayo wamepatiwa vyeti ambavyo vitaweza kuwatambulisha ushiriki wao kwenye mafunzo hayo, ambayo yametajwa kusaidia kuongeza idadi ya madereva wenye weledi wa usafirishaji salama wa kemikali na mizigo mingine hatarishi.

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.