MKEMIA MKUU WA SERIKALI

Karibu Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, kituo chako namba moja kwa uchunguzi wa kimaabara wa sampuli zinazohusiana na sayansi jinai ili kuwezesha uchunguzi wa jinai, hivyo kuhakikisha upatikanaji wa haki na utawala wa Sheria, sampuli zinazohusiana na kilimo na bidhaa za viwandani ili kubaini usalama na ubora, sampuli zinazohusiana na uhalali wa mtoto kwa wazazi au utambuzi wa jinsi tawala ili kusaidia utatuzi wa masuala mbalimbali kwenye jamii na sampuli zinazohusiana na mazingira na usalama mahali pa kazi kwa ajili ya kulinda afya na mazingira.Soma Zaidi>>

SAA ZA KAZI

OFISI ZINAFUNGULIWA KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 ALASIRI

KUANZIA JUMATATU HADI IJUMAA ISIPOKUWA SIKU ZA SIKUKUU

 

SENSA YA WATU NA MAKAZI

MITANDAO YA KIJAMII

Twitter icon
Facebook icon
YouTube icon
Instagram icon
 • WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB) (WA TANO KUTOKA KULIA) AKIWA PAMOJA NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI NA MENEJIMENTI YA MAMLAKA MARA BAADA YA KUIZINDUA BODI TAREHE 13 AGOSTI, 2021 KATIKA UWANJA WA JENGO LA MKEMIA, DAR ES SALAAM.

 • WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB) (WA TANO KUTOKA KULIA) AKIWA PAMOJA NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA PILI YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI MARA BAADA YA KUIZINDUA BODI HIYO TAREHE 13 AGOSTI, 2021 KATIKA UWANJA WA JENGO LA MKEMIA, DAR ES SALAAM

 • WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (KATIKATI) AKIMKABIDHI MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI, PROFESA ESTHER HELLEN LUGWISHA (PICHA YA KWANZA, KUSHOTO) NA KATIBU WA BODI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO (PICHA YA PILI) SHERIA NA KANUNI ZAKE ZINAZOSIMAMIWA NA MAMLAKA IKIWA NI ISHARA YA KUIZINDIA RASMI BODI HIYO.

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO, AKITOA HOTUBA YAKE KABLA YA KUMKARIBISHA MGENI RASMI WAKATI WA UZINDUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA PILI YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI AMBAYO ILIZINDULIWA NA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB) KWENYE OFISI ZA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DAR ES SALAAM.

 • WAZIRI WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB) (KULIA) AKIONGEA WAKATI ANAZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA PILI YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI TAREHE 13 AGOSTI, 2021 MBELE YA WA JENGO LA MKEMIA, DAR ES SALAAM. KUSHOTO (WALIOKAA) NI MWENYEKITI WA BODI HIYO, PROFESA ESTHER HELLEN JASON NA MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO.

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT FIDELICE MAFUMIKO (KATIKATI WALIOKAA) AKIWA PAMOJA NA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA WALIOFANYA VIZURI KWENYE MASOMO YA KEMIA,BIOLOJIA NA FIZIKIA MARA BAADA YA KUWAKABIDHI ZAWADI TAREHE 10 JULAI 2021.

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO (KUSHOTO), AKIWAKABIDHI VYETI WALIMU WALIOFANYA VIZURI KWA KUWEZESHA KUTOA WANAFUNZI WALIOONGOZA KWA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA KWA MASOMO YA KEMIA, BAIOLOJIA NA FIZIKIA TAREHE 10 JULAI 2021.

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO (KUSHOTO), AKIWAKABIDHI ZAWADI ZA VYETI WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KWA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA KATIKA MASOMO YA KEMIA,BAIOLOJIA NA FIZIKIA KATIKA HAFLA ILIYOANDALIWA NA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI TAREHE 10 JULAI 2021.

 • WALIMU NA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA KEMIA, BAIOLOJIA NA FIZIKIA WAKIMSIKILIZA MKEMIA MKUU WA SERIKALI (HAYUPO PICHANI) WAKATI AKIFUNGUA HAFLA FUPI YA KUTOA ZAWADI KWA WALIMU NA WANAFUNZI HAO ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MKEMIA HOUSE TAREHE 10 JULAI 2021.

 • Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya(DCEA),Gerald Kusaya akisikiliza maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Sabanitho Mtega na Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kulia) kuhusu majukumu ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kutembelea Banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara(Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 • Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya(DCEA),Gerald Kusaya akisaini Kitabu cha wageni katika Banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali alipotembelea Banda hilo katika maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Sabanitho Mtega na Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kulia).

   

 • Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo na Kamishna wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (hayupo pichani) walipotembelea banda la Mamlaka katika Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya yaliyofikia kilele jijini Dodoma.

 • Watumishi wa Mamlaka walioshiriki Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya jijini Dodoma

 • Mkemia Mkuu wa Serikali, (wa pili kulia) akimsikiliza Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Betha Mamuya (kulia) mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka katika Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya yaliyofanyika leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias

 • Mkemia Mkuu wa Serikali, (katikati) na Msajili wa Baraza la Wafamasia, Elizabeth Shekalaghe (kulia) wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya (kushoto) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya jijini Dodoma leo

 • Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kushoto) wakati akimuonesha takwimu za uchunguzi wa dawa mbalimbali za kulevya zilizochunguzwa katika maabara za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miaka sita wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani tarehe 26 Juni, 2021 ambapo Waziri Simbachawene alishiriki kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambapo kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Nyerere Square, mkoani Dodoma. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya.

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO (ALIYEKAA KATIKATI), MENEJA WA OFISI YA KANDA YA KASKAZINI, CHRISTOPHER ANYANGO (WA PILI KUSHOTO), HAKIMU WA MAHAKAMA YA WILAYA YA ARUSHA, MHE. PAMELA MEENA (WA PILI KULIA) WAKIWA PAMOJA NA WADAU WENGINE WA MAMLAKA MARA BAADA YA KUMALIZA KIKAO NA WADAU HAO KATIKA OFISI YA KANDA YA KASKAZINI ILIYOPO SEKEI JIJINI ARUSHA.

 • MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAWAKALA WA FORODHA MPAKA WA NAMANGA, ISMAIL KILASI (PICHA YA CHINI) AKIWASILISHA HOJA KUHUSIANA NA MABORESHO YA HUDUMA ZA MAMLAKA WAKATI WA KIKAO NA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KILICHOFANYIKA  KATIKA OFISI ZA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA KANDA YA KASKAZINI ILIYOPO  JIJINI ARUSHA.

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO (WA PILI KUSHOTO) AKIELEKEZA MABORESHO YANAYOHITAJIKA KUFANYWA  KWENYE MAABARA YA KIWANDA CHA TPPL ILI KUKIDHI VIWANGO VINAVYOHITAJIKA KWA MUJIBU WA SHERIA YA USIMAMIZI WA KEMIKALI

 • MSIMAMIZI WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) KATIKA MPAKA WA SIRARI, JACKSON MOSHA(KUSHOTO) AKIONGEA WAKATI WA KIKAO CHA MKEMIA MKUU WA SERIKALI NA WATUMISHI WA TAASISI ZA SERIKALI KATIKA MPAKA WA SIRARI NA WADAU WA MAMLAKA KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO MPAKANI HAPO

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO (WA PILI KUSHOTO), MKURUGENZI WA HUDUMA ZA TAASISI, EVACLOTIDA KAPINGA (KUSHOTO) NA KAIMU MENEJA WA OFISI YA KANDA YA ZIWA, DANSTAN MKAPA (WA PILI KULIA) WAKIMSIKILIZA MKAGUZI WA KEMIKALI WA MAMLAKA KATIKA MPAKA WA SIRARI, FAZIRI SHEDAN (KULIA) MARA BAADA YA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI YA KUTEMBELEA MPAKA WA SIRARI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA UKAGUZI WA KEMIKALI.

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO (KUSHOTO) NA WATUMISHI WA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI WAKIKAGUA MIONGOZO MBALIMBALI INAYOTUMIKA KATIKA MAABARA YA KIWANDA CHA KILIMANJARO BIOCHEM KATIKA KUFANYA UCHUNGUZI WA KIMAABARA KWA AJILI YA KUHAKIKISHA BIDHAA WANAYOZALISHA INATOKA KATIKA UBORA UNAOKIDHI MAHITAJI YA WATUMIAJI WA BIDHAA HIYO.  

 • MKEMIA MKUU WA SERIKALI, DKT. FIDELICE MAFUMIKO (KULIA) NA MENEJA WA OFISI YA KANDA YA KASKAZINI, CHRISTOPHER ANYANGO (WA PILI KULIA) WAKIMSIKILIZA MENEJA UZALISHAJI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA SPIRIT CHA KILIMANJARO BIOCHEM LTD, KRISHNA GOUD (KUSHOTO) AKIWAELEZA NAMNA UZALISHAJI WA SPIRIT UNAVYOFANYIKA KATIKA KIWANDA HICHO WAKATI WA UKAGUZI ULIOFANYIKA  TAREHE 12 JUNI, 2021 MOSHI, KILIMANJARO.

 • Washiriki wa mafunzo ya Usimamizi salama wa kemikali yaliyowahusisha Wasimamizi wa Kemikali kutoka makampuni yanayosafirisha, kuuza na kuingiza Kemikali nchini wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Bw.Sabanitho Mtega (hayupo picha) wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo jana.

 • Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega (kulia) akifungua mafunzo ya siku mbili kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa serikali kwa wasimamizi wa Kemikali kutoka katika makampuni yanayosafirisha,kuingiza na kuuza  Kemikali ikiwa ni mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujua namna bora ya usimamizi wa kemikali. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Gerald Melliyo. Mafunzo hayo yalifunguliwa jana tarehe 20 Mei, 2021 katika Ukumbi wa Hazina, Dar es Salaam.

 • Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), Msimamizi wa Kituo cha Taifa cha Kuratibu Matukio ya Sumu (NPCC), Yohana Goshashy (kulia) na Meneja wa Fedha wa Mamlaka, Matrida Lugenge (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo mara baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufungua mafunzo hayo jana tarehe 20 Mei, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Bunge, Dar es Salaam

 • Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akiongea na Wataalam wa afya wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wataalam hao lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo na utambuzi wa matibabu kwa waathirika wa matukio ya sumu yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam tarehe 20 -21 Mei, 2021. Kulia ni Msimamizi wa kituo cha Kuratibu Matukio ya sumu, Yohana Goshashy.

 • Afisa Sheria kutoka Mamlaka, Abeid Kafunda, akielezea vifungu mbalimbali vya Sheria ya Udhibiti wa Vinasaba vya Binadamu ambavyo vinawataja madaktari kama moja ya wadau wa uchukuaji wa sampuli na wanavyoweza kuvitumia kushirikiana na Mamlaka katika usimamizi wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara kwa masuala ya kijamii, jinai na tiba

 • Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka Mamlaka, Ramadhan Nauja (kushoto) akiwasilisha mada kuhusiana na taratibu za uchunguzi wa vinasaba na namna ya uchukuaji, uhifadhi na udhibiti wa sampuli za Vinasaba vya Binadamu kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara kwa wanafunzi wa mwaka wa nne na tano wa masomo ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi yaliyofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Bugando, Mwanza.

 • Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mkemia Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti na Kaimu Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki wakikagua maeneo mbalimbali ya kuhifadhi kemikali katika Bandari Kavu ya PMM ambapo waliongozwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano kwa Umma wa PMM, Deogratias Chacha (kushoto).

Karibu Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, kituo chako namba moja kwa uchunguzi wa kimaabara wa sampuli zinazohusiana na sayansi jinai ili kuwezesha uchunguzi wa jinai, hivyo kuhakikisha upatikanaji wa haki na utawala wa Sheria, sampuli zinazohusiana na kilimo na bidhaa za viwandani ili kubaini usalama na ubora, sampuli zinazohusiana na uhalali wa mtoto kwa wazazi au utambuzi wa jinsi tawala ili kusaidia utatuzi wa masuala mbalimbali kwenye jamii na sampuli zinazohusiana na mazingira na usalama mahali pa kazi kwa ajili ya kulinda afya na mazingira. Soma Zaidi>>

Error message

Notice: Undefined offset: 1 in counter_get_browser() (line 71 of /var/www/gclawebsite/sw/sites/all/modules/counter/counter.lib.inc).

Dhima Dira na Misingi Mikuu

 • Dira

Kuwa maabara ya uchunguzi yenye hadhi duniani kwa ajili ya kushughulikia maswala ya afya, ustawi wa jamii na mazingira

 

 

 • Dhima

Kutoa huduma bora za uchunguzi wa kimaabara na udhibiti zenye ubora na gharama nafuu kwa serikali, taasisi, asasi na umma kwa ujumla kwa dhumuni la kulinda afya ya binadamu na mazingira

 

 • Misingi Mikuu

 

Katika kutoa huduma bora tutaongozwa na misingi mikuu minane ambayo ni :- Kutoa huduma bora , Weledi , Uwajibikaji ,Moyo wa Ushirikiano,

Utofauti,Uwazi,Uaminifu kwa Serikali,Uadilifu na  Maadili na utendaji wa msingi ya kimaadili.

 • Sensa ya Watu na Makazi

Haki Miliki©2022 Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Haki Zote Zimehifadhiwa.

Imetengenezwa na Kusanifiwa na Wataalamu wa TEHAMA wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali