Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

GCLA YAPONGEZWA KWA KUSAIDIA UPATIKANAJI WA HAKI

Imewekwa: 29 Jan, 2025
GCLA YAPONGEZWA KWA KUSAIDIA UPATIKANAJI WA HAKI

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi kubwa inayofanya katika upatikanaji wa haki Jinai nchini Tanzania huku akifurahishwa na utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka kwa ujumla.

Prof. Gabriel ametoa pongezi hizo katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, jiji Dodoma wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo amesema GCLA inafanyakazi kubwa  ambayo Serikali inatambua na kuiomba Mamlaka iwekeze nguvu kubwa kujitangaza katika vyombo vya habari

“GCLA inafanyakazi kubwa sana katika upatikanaji wa haki jinai nchini lakini vilevile kwenye utekelezaji wa majukumu yake kwa ujumla, wito wangu naomba wajikite kujitangaza kwenye vyombo vya habari ili wananchi wajue kazi kubwa wanayoifanya” alisema Prof. Gabriel

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias, amesema katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2025 inayomalizika mwezi Desemba, Serikali imewekeza rasilimali za kutosha hali iliyosaidia kufanyika maboresho makubwa katika utendaji kazi wa Mamlaka

“Serikali imeboresha kwa kiwango kikubwa sana utendaji wa Mamlaka kwa kununua Mitambo ya Kisasa ambapo tofauti na awali kwa sasa matokeo ya uchunguzi yanatoka kwa wakati bila kuchelewa, kuelekea Dira ya Taifa 2025 maboresho makubwa zaidi yanafanyika katika mifumo ikiwemo kuunganishwa kwa mifumo yaTEHAMA kwa wadau wa haki jinai ikiwemo Jeshi la Polisi ili kuwa na uwezo wa kufuatilia mwenendo wa sampuli kutoka inapofika mpaka matokeo yanapotoka” alisema Elias.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi kubwa inayofanya katika upatikanaji wa haki Jinai nchini Tanzania huku akifurahishwa na utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka kwa ujumla.

Prof. Gabriel ametoa pongezi hizo katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, jiji Dodoma wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo amesema GCLA inafanyakazi kubwa sana ambayo Serikali inatambua na kuiomba Mamlaka iwekeze nguvu kubwa kujitangaza katika vyombo vya habari