Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala
Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala
Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo: -
- Utekelezaji wa Sera na Mikakati ya Rasilimali Watu;
- Kusaidia kutafsiri na utekelezaji wa Sheria za Utumishi wa Umma, Sheria ya Wakala wa Serikali na Kanuni zake, Miongozo ya kiutumishi na Sheria za Kazi;
- Kusimamia uhusiano na ustawi wa Watumishi ikiwemo usalama wa afya, malipo ya uzeeni, michezo na utamaduni;
- Kuratibu na kusimamia Masjala, Kumbukumbu za Ofisi na huduma za Uongozi na Usambazaji wa Vifurushi na Nyaraka;
- Kusimamia huduma za ulinzi, usafiri na matumizi ya ofisi kwa ujumla;
- Usimamizi wa ujumla wa matengenezo ikiwemo matengenezo ya vifaa vya ofisi, majengo na maeneo ya ofisi;
- Kutekeleza masuala mtambuka ikiwemo Jinsia, Kuzuia Rushwa, Maadili, wasiojiweza, VVU/UKIMWI na mambo mengine yanayohusiana na hayo;
- Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Ushiriki wa Sekta Binafsi katika Shughuli za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
- Kuratibu na kusimamia masuala yanayohusu ushiriki wa Watumishi katika Shughuli za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kuwezesha mafunzo na maendeleo ya Rasilimali Watu;
- Kuandaa na kutekeleza mipango ya Rasilimali Watu;
- Kusimamia mishahara na malipo ya mishahara; na
- Kuandaa mipango na bajeti ya mishahara ya Watumishi ya mwaka.