Ofisi za Kanda
Ofisi za Kanda
Majukumu ya Ofisi za Kanda
- Kufanya uchunguzi wa kimaabara na kutoa ushauri kwa Serikali katika masuala yanayohusu vyakula, dawa, mazingira, jinai, vinasaba, dawa za kulevya, na kwa lengo la kulinda afya za binadamu na mazingira;
- Kuchukua na kupokea sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara katika mikoa yote inayounda Kanda husika;
- Kusajili na kukagua Maabara za Kemia, Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu, na wadau wa kemikali kwa mujibu wa Sheria zinazosimamiwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kusimamia na kufanya ukaguzi endelevu kwa wadau wa kemikali, Maabara za Kemia, Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu kama ilivyoelekezwa kisheria;
- Kusimamia mipaka yote inayoingiza na kutoa kemikali nchini ili kulinda usalama wa nchi dhidi ya uingizaji wa kemikali hatarishi, bashirifu na kemikali zisizohitajika au zilizopigwa marufuku kuingia nchini;
- Kutoa ushahidi wa kitaalam mahakamani katika mashauri yanayohusisha taarifa za matokeo ya uchungizi wa kimaabara;
- Kupokea maombi na kupendekeza usajili wa wadau wa kemikali, Maabara za Kemia, Sayansi Jinai na Vinasaba; na
- Kutoa Mafunzo kwa Wadau wa Maabara za Kemia, Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu na wadau wa kemikali.