Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Sehemu ya Maabara ya Sayansi Jinai Kemia

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo: -

  • Kuchunguza dawa za kulevya kama bangi, mirungi, heroini, kokeini kwa ajili ya utambuzi wa kiwango na aina ya dawa hizo;
  • Kuchunguza unga na vidonge ili kutambua kuwepo au kutokuwepo kwa dawa za kulevya zinazohusiana na makosa ya jinai;
  • Kuchunguza vimiminika ili kubaini kuwepo au kutokuwepo kwa dawa za kulevya zinazohusiana na makosa ya jinai;
  • Kuchunguza vyakula ili kubaini kuwepo au kutokuwepo kwa dawa za kulevya zinazohusiana na makosa ya jinai
  • Kuchunguza sampuli za baiolojia kama vile mkojo, jasho, mate, nywele na damu ili kubaini kuwepo au kutokuwepo kwa dawa za kulevya zinazohusiana na makosa ya jinai;
  • Kubaini kiwango cha dawa za kulevya kwa ajili ya makossa ya jinai na yasiyo ya jinai;
  • Kuchunguza mabaki kutoka katika majanga ya moto ili kubaini chanzo cha moto huo
  • Kuchunguza vilipuzi na mabaki ya vilipuzi ili kubaini aina ya kemikali zilizotumika katika kutengeneza vilipuzi hivyo;
  • Kuchunguza mabaki ya silaha ya moto iliyotumika ili kubaini aina ya silaha iliyotumika katika tukio;
  • Kuchunguza mabaki ya vioo ili kulinganisha na vioo vilivyopatikana kwenye eneo la tukio
  • Kuchunguza mabaki ya udongo na vumbi ili kubaini wahalifu kwa kulinganisha naudongo au vumbi lililopatikana katika eneo la tukio;
  • Kuchunguza rangi ili kubaini wahalifu kwa kulinganisha narangi iliyopatikana katika eneo la tukio;
  • Kuchunguza nyaraka za kughushi na fedha bandia ili kutambua nyaraka na fedha halisi;
  • Kutoa ushahidi wa kitaalam mahakamani kuhusiana na uchunguzi wa kimaabara;
  • Kutoa elimu kwa wataalam juu ya tatatibu za uchukuaji na usimamizi wa sampuli zinazohusiana na Maabara ya Sayansi Jinai Kemia;
  • Kufanya utafiti kwa masuala yanayohusiana na Maabara ya Sayansi Jinai Kemia;
  • Kufanya uchunguzi wa sampuli zinazohusiana na sayansi jinai kemia zenye maslahi ya kijamii na kitaifa;
  • Kutayarisha, kutathmini na kufanya mapitio ya mbinu za uchunguzi wa Maabara ya Sayansi Jinai Kemia;
  • Kutayarisha,kutathmini na kufanya mapitio ya taratibu ya uchunguzi wa Maabara ya Sayansi Jinai Kemia;
  • Kushiriki kwenye uchunguzi wa kujipima umahiri ili kuwajengea uwezo na ujuzi wataalamu wa Maabara ya Sayansi Jinai Kemia; na
  • Kutoa ushauri wa kitaalam juu ya masuala yanayohusiana na Maabara ya Sayansi Jinai Kemia.