Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Sehemu ya Maabara ya Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo: -

  • Kuchunguza sampuli za kibaiolojia zilizopatikana katika maeneo ulipotokea uhalifu;
  • Kufanya uchunguzi wa sampuli za kibaiolojia, nguo, vitu mbalimbali, silaha za moto na za jadi kwa ajili ya utambuzi wa binadamu unaohusiana na makosa ya mauaji, unyang’anyi, ubakaji na uhalifu mwingine wowote;
  • Kufanya uchunguzi wa vinasaba vya binadamu kwa ajili ya utambuzi wa binadamu wakati wa majanga;
  • Kufanya uchunguzi wa vinasaba vya binadamu ili kubaini mahusiano ya kindugu na kusaidia kuzuia biashara haramu ya kusafisha watu na wahamiaji haramu;
  • Kufanya uchunguzi wa vinasaba vya binadamu ili kubaini jinsi tawala kwa watu wenye jinsi tata;
  • Kufanya uchunguzi wa vinasaba vya binadamu unaosaidia matibabu ya kibingwa ili kuwezesha hatua za awali katika upandikizaji figo kwa wagonjwa
  • Kufanya utambuzi wa sampuli za viumbe hai visivyotambulika;
  • kufanya uchunguzi wa vinasaba ili kubaini mahusiano ya mtoto kwa wazazi
  • Kutoa ushahidi wa kitaalam mahakamani katika masuala yanayohuisiana na uchunguzi wa vinasaba;
  • Kutoa elimu kwa wataalam kuhusiana na usimamizi na udhibiti wa mnyororo wa sampuli za vinasaba;
  • Kufanya utafiti na kutoa ushauri juu ya masuala yanayohusiana na uchunguzi wa sayansi jinai baiolojia na vinasaba;
  • Kufanya uchunguzi wa sampuli za baiolojia na vinasaba zinazohusiana na maslahi ya jamii na Taifa;
  • Kutayarisha, kutathmini na kufanya mapitio ya miongozo ya uchunguzi wa Maabara ya Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba;
  • Kutayarisha, kutathmini na kufanya mapitio ya taratibu ya uchunguzi wa Maabara ya Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba;
  • Kushiriki kwenye uchunguzi wa kujipima umahiri ili kuwajengea uwezo na ujuzi wataalamu wa Maabara ya Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba;
  • Kuanzisha na kuratibu uanzishaji na usimamizi wa Kanzidata ya Taifa ya Vinasaba vya Binadamu;
  • Kutekeleza Mikataba ya Kimataifa iliyoridhiwa inayohusiana na sayansi jinai
  • Kutayarisha Miongozo ya usimamizi na udhibiti wa taarifa za vinasaba vya binadamu; na
  • Kutoa mafunzo maalum kuhusu usimamizi wa sampuli za vinasaba na takwimu kwa wataalam wa Maabara teule za Vinasaba