Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini
Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini
Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo: -
- Kutoa mwongozo wa kitaalam na kusaidia uandaaji na utekelezaji wa mpango mkakati na bajeti ndani ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kuratibu maandalizi ya bajeti ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa “dash board” ya Mamlaka ikiwemo viashiria vya kiutendaji vya kifedha na visivyo vya kifedha.
- Kupitia viashiria na viwango vya utendaji;
- Kufuatilia na kutathmini Mipango Biashara na Mipango Mikakati ya Muda wa Kati;
- Kuratibu uandaaji wa ripoti ya ufuatiliaji na tathmini;
- Kutathmini matokeo ya miradi na programu zinazofanywa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kuratibu utafiti wa utaoji huduma na kuishauri Menejimenti;
- Kutathmini utendaji wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ikiwemo mipango mkakati na hatua za utekelezaji wa miradi;
- Kuratibu uandaaji wa ripoti za utendaji za Robo, Nusu na Mwaka;
- Kuandaa, kutekeleza na kuhuisha Taratibu za Utendaji kazi za Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini; na
- Kushirikiana na Wadau katika kuandaa mpango mkakati na taratibu za bajeti ndani ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikal