Kitengo cha Huduma za Sheria
Kitengo cha Huduma za Sheria
Kitengo kinafanya kazi zifuatazo:
- Kutoa ushauri na msaada kwa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti juu ya tafsiri ya Sheria, masharti ya mikataba, makubaliano, mikataba ya ununuzi, dhamana, barua ya ahadi, mikataba ya ushauri elekezi, aina mbalimbali ya makubalinao na nyaraka za kisheria;
- Kupitia na kuandaa taratibu za kisheria za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kushauri maeneo ya kuboresha;
- Kupitia ripoti na maoni ya kisheria juu ya masuala yanayohusu madai ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye vikao vya Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti;
- Kuhakikisha mahitaji ya kisheria na kikanuni yanatekelezwa.
- Kushiriki katika majadiliano na mikutano ambayo inahitaji utaalam wa kisheria;
- Kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu kesi za madai, jinai na madai mengine yanayoihusu Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kutunza na kuhakikisha usalama wa nyaraka zote za kisheria za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kuandaa na kupitia nyaraka mbalimbali za kisheria kama miongozo, matangazo, makubaliano na hati za uhamisho; na
- Kuwezesha mashahidi wa wataalam kuhudhuria kesi mahakamani