Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Shenda, Kata ya Masumbwe Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita mara baada ya kufika katika Kijiji hicho kwa ajili ya kufanya ukaguzi katika mialo ya wachimbaji wa dhahabu katika Kijiji cha Shenda Novemba 30, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa kofia nyeusi) akikagua moja ya mialo inayotumika kuchenjua dhahabu katika Kijiji cha Shenda, Kata ya Masumbwe ambapo wachimbaji hao wanatumia kemikali ya Zebaki katika shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.
Mkemia Mkuu wa Serikali (aliyevaa kofia nyeusi) akiangalia kipande cha dhahabu kilichopatikana baada ya kuchenjuliwa kwa kutumia kemikali ya Zebaki kwenye eneo la mialo alilokagua katika Kijiji cha Mwakitolyo kilichopo katika Kata ya Mwakitolyo Mkoa wa Shinyanga Disemba 2, 2024
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko na Meneja wa Kanda ya Ziwa, wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Wachimbaji wadogo Mwakitolyo, Matemula Lameck (aliyevaa koti jeusi) akieleza namna shughuli zao za uchimbaji katika mialo iliyopo kijijini hapo unavyofanyika na namna mafunzo ya matumizi salama ya kemikali ya Zebaki yaliyowasaidia katika kujilinda wakati wa uchenjuaji wa dhahabu.
Wadau wa kemikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kwa wadau wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 28,2024.
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerard Meliyo (aliyesimama), akiwasilisha mada kuhusu Sheria na Kanuni za Usimamizi wa Kemikali za Viwandani na Majumbani katika mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kwa wadau wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 28,2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Musa Kuzumila (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kwa wadau wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 28,2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Musa Kuzumila, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa Wadau wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 28,2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Musa Kuzumila (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na wadau wa kemikali walioshiriki mafunzo ya matumizi salama ya kemikali pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Meneja wa Mamlaka Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na washiriki wa mafunzo kuhusu majukumu ya Mamlaka kwa kundi la Mawakala wa Forodha katika Kanda ya Mashariki.