Sehemu ya Usajili na Ukaguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu
Sehemu ya Usajili na Ukaguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu
Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:
- Kutayarisha Miongozo, Mipango ya ukaguzi na dodoso kwa ajili ya usajili na ukaguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu;
- Kuratibu na kufanya ukaguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu;
- Kutoa vyeti au leseni za usajili wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu;
- Kutunza na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu;
- Kuratibu Mikutano ya Kamati ya Kitaalam ya Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu;
- Kuratibu na kutekeleza Itifaki ya Montreal inayohusu kulinda tabaka la Ozoni;
- Kufanya mafunzo maalum kwa Wakaguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu na kuwatangaza kwenye Gazeti la Serikali;
- Kupendekeza Kanuni mpya na kufanya mapitio ya Kanuni zinazohusiana na kemikali na maabara za kemia;
- Kuratibu uandaaji na utekelezaji wa sera za kemikali, tafiti au programu za kitaifa na kimataifa; na
- Kufuatilia utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Udhibiti wa Vinasaba vya Binadamu na Kanuni zake.