Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Dhima Dira na Misingi Mikuu

1.DHIMA na DIRA

  • Dira

     Kuwa maabara ya uchunguzi yenye hadhi duniani kwa ajili ya kushughulikia maswala ya afya, ustawi wa jamii na mazingira

  • Dhima

Kutoa huduma bora za uchunguzi wa kimaabara na udhibiti zenye ubora na gharama nafuu kwa serikali, taasisi, asasi na umma kwa ujumla kwa dhumuni la kulinda afya ya binadamu na mazingira.

2.MISINGI MIKUU

Katika kutoa huduma bora Mamlaka (GCLA) itaongozwa na misingi mikuu minane ambayo ni:

  • Kutoa Huduma Bora- Tunaamini ikatika kutoa huduma bora na kumridhisha mteja. Tutatumia rasilimali tulizonazo kwa kufuata utaalam na utoaji huduma bora. Tutakuwa wasikivu kulingana na mahitaji na matakwa ya mteja. Jina la Mamlaka ya Maabra ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye soko litaendana na ubora, uwajibikaji na umahiri.
  • Tunaamini katika umahiri na weledi katika jitihada zetu za kuokoa na kulinda uhai.
  • Tunaamini katika uwajibikaji na kuwajibika kwa matendo yetu wakati wa kutekeleza majukumu yetu
  • Utaalam – Tunaamini katika moyo wa ushirikiano ili kuendelea kutoa huduma bora na zenye ufanisi. Mchango wa kila mmoja utapewa kipaumbele na kuthaminiwa. Timu zitaundwa na wataalam toka ngazi mbalimbali za kiuongozi na kisayansi. Kwa muktadha huo tutashirikiana na wataalam wenzetu, washirika, wakati tukiheshimu mawazo mtambuka na misingi mbalimbali ya majadiliano kuhusu njia mbadala na mwisho kwa pamoja kufikia suluhisho bora la kuendesha Maabara hii ya Serikali.
  • Utofauti – Tunaamini katika utofauti. Sera zetu zitaakisi imani ya usawa na haki kwenye kuweka mazingira mazuri kwa watu wenye misingi tofauti ya kiutamaduni, elimu na jinsi, kufanya kazi kulingana na taaluma zao na kuridhika na kazi.
  • Uwazi – Tunaamini katika kubadilishana taarifa ndani na nje ya Taasisi.Tutajitahidi kutambua ushirikishwaji katika kufanya maamuzi. Tutawasiliana na wateja na wadau wetu kwa kujituma na kuwajibika.
  • Uaminifu kwa Serikali – Tutakuwa waaminifu kwa Serikali iliyoko madarakani na kutekeleza Sera na maelekezo ya kisheria yanayotolewa na Waziri na viongozi wengine wa Serikali
  • Uadilifu-Tukiwa kama Mamlaka yenye dhamana ya kusimamia uchunguzi wa sayansi jinai, huduma za vinasaba, usajili wa kemikali, wadau na maabara, kila mtumishi wa Mamlaka ana wajibu wa kuonyesha kiwango cha juu cha uadilifu ili kutoa msukumo wa kujiamini na kuaminiwa.