Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Kitengo kinafanya kazi zifuatazo:
- Kuandaa na kutekeleza Mpango wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma;
- Kusimamia uratibu wa programu za vyombo vya habari;
- Kuratibu maandalizi ya Taarifa kwa Vyombo vya Habari, Hotuba na Makala;
- Kuhamasisha na kutangaza huduma za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa Umma;
- Usimamizi na uhuishaji wa Tovuti ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kuratibu ushiriki wa matukio na maonesho mbalimbali;
- Kuratibu maandalizi ya utengenezaji wa Kalenda, Makala, Vipeperushi, Taarifa kwa mteja na Jarida la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kuratibu usimamizi wa malalamiko ya mteja kwenye Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kuandaa, kutekeleza na kuhuisha taratibu za utendaji kazi za Uhusiano kwa Umma;
- Kuratibu mafunzo au uhamasishaji wa huduma kwa mteja;
- Ufuatiliaji wa shughuli za matangazo na kujitangaza; na
- Kupitia, kushauri na kutelekeza mpango wa masoko na mikakati ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.