Kitengo cha Udhibiti Ubora na Usimamizi wa Vihatarishi
Kitengo cha Udhibiti Ubora na Usimamizi wa Vihatarishi
Kitengo hiki kinafanya kazi zifuatazo:
- Kutekeleza mifumo ya Usimamizi wa Ubora na matakwa ya Ithibati za Maabara;
- Kuratibu na kufanya ukaguzi wa ndani na nje ya Usimamizi wa Mifumo ya Ubora;
- Kuratibu na kufanya mapitio ya mara kwa mara ya usimamizi wa Mifumo ya Ubora
- Kuratibu na kusimamia mipango ya Usimamizi wa Mifumo ya Ubora, kufanya ufuatiliaji, kutoa mafunzo na maboresho ya mara kwa mara;
- Kufanya ufuatiliaji na mapitio ya utekelezaji wa Sheria, Viwango vya Mifumo ya Ubora vya Kitaifa na Kimataifa;
- Kusimamia uandaaji, utekelezaji na uidhinishwaji na utunzwaji wa taratibu za uchunguzi wa kimaabara, kuratibu programu za umahiri za uchunguzi wa kimaabara na Ithibati za Maabara;
- Kuandaa, kusimamia na kufanya tathmini ya utekelzaji wa Rejesta ya Usimamizi wa Vihatarishi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kutunza na kufanya mapitio ya utekelzaji wa Rejesta ya Usimamizi wa Vihatarishi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
- Kutoa mafunzo kwa wataalam wa Mamlaka juu ya vihatarishi; na
- Kutayarisha, kutumia na kuhuisha taratibu za Ukaguzi wa vihatarishi.