Kitengo TEHAMA na Takwimu
Kitengo TEHAMA na Takwimu
Kitengo hiki kinafanya kazi zifuatazo: -
- Kusimamia na kupanga mtandao kwa matumizi ya sasa na baadae pamoja na kutengeneza mifumo na kanzidata kutegemeana na mahitaji
- Usimamizi, utunzaji na urudishaji wa taarifa wakati wa utengenzaji na utekelezaji wa majaribio ya mifumo mara kwa mara;
- Usimamizi wa usimikaji, ufungaji, uboreshaji, na uhamishaji wa programu ya kanzidata na matoleo mapya yanayohusiana na programu hiyo pia kuhamisha taarifa kutoka Server za zamani kupeleka Server mpya;
- kuidhinisha utekelezaji wa mabadiliko ya usanidi kwa mitandao ya nje na ndani;
- Kuandaa na kuelekeza sera ya TEHAMA na mipango mkakati ya maendeleo inayohusiana na Miundombinu ya Mtandao;
- Kutoa uangalizi wa kiufundi na mwongozo kwa mifumo na miundombinu yote ya kituo cha data;
- Kuwezesha usambazaji wa maarifa yanayohusiana na TEHAMA kwa Watumishi wa Mamlaka;
- Kusaidia katika kubuni na uunganishaji wa mifumo na kuhakikisha utangamano wa mifumo iliyopo na miundombinu ya mtandao;
- Usimamizi wa mchakato wa mabadiliko ya usanidi na kutoa taarifa ya kukatika kwa mtandao;
- Kutengeneza zana na mbinu rahisi za ufikiaji wa data, takwimu na ripoti;
- Kuwezesha ukusanyaji, uchambuzi na kutayarisha ripoti juu ya takwimu za Mamlaka;
- Kuratibu ukusanyaji na uchambuzi wa data na uandaaji wa takwimu zinazohusiana na sekta;
- Kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa nyaraka zinazohusiana na usalama wa TEHAMA
- Kuchambua na kutafsiri takwimu ili kutambua umuhimu kuhusiana na vyanzo vya taarifa; na
- Kutunza data za Mamlaka