Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

MKEMIA MKUU WA SERIKALI APOKEA TUZO YA USHINDI WA MAONESHO YA GEITA

Imewekwa: 19 Oct, 2023
MKEMIA MKUU WA SERIKALI APOKEA TUZO YA USHINDI WA MAONESHO YA GEITA

Akiongea wakati wa kupokea tuzo hiyo, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewapongeza watumishi wote walioshiriki maonesho hayo na kufanikisha kuibuka na ushindi ambao umeiletea sifa Mamlaka ikiwa ni moja ya wadau muhimu katika sekta ya madini.

“Nawapongeza watumishi walioshiriki maonesho ya Sita ya Teknolojia ya madini mkoani Geita na kuwezesha kuibuka washindi wa kwanza. Hii ni sifa nzuri kwetu kama Mamlaka na imetokana na kujituma kwenu na kutambua kwamba mlikuwa mnaiwakilisha Mamlaka na matokeo yake sifa imekuja kwetu wote kama taasisi. Hii iwe ndio hamasa yetu kutambua kwamba tukipewa kazi ya kufanya basi tuifanye kwa kujituma, weledi na umakini na tukifanikiwa sifa inakuja kwetu wote na tukifanya vibaya pia inakuwa inatuhusu wote kama Mamlaka” alisema.

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali, ameelekeza kwamba watumishi wote walioshiriki Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini Geita na kuleta ushindi huo kupatiwa vyeti vya kutambua mchango wao katika kuwezesha kupatikana kwa ushindi huo.