Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

WANANCHI WAASWA KUJIKINGA NA MADHARA YA KEMIKALI ZA ASILI

Imewekwa: 07 Aug, 2024
WANANCHI WAASWA KUJIKINGA NA MADHARA YA KEMIKALI ZA ASILI

Wananchi wa Kanda ya Kaskazini wamehimizwa kutumia fursa ya maonesho ya Wakulima Nane nane kutembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali  ili kujifunza na kupata elimu ya kujikinga na madhara ya kemikali

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Eliamini Mkenga kwenye maonesho ya Wakulima Nane nane yanayofanyika katika viwanja vya Themi, Njiro, Jijini Arusha.

Akiongea na wananchi waliotembelea banda la Mamlaka, Mkenga ametoa wito kwa wananchi hususani wakulima na wachimbaji wa madini kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo na kutembelea banda la Mamlaka ili kupata huduma mbalimbali na elimu juu ya huduma zinazotolewa na Mamlaka zinazohusiana na uchunguzi wa kimaabara na Usimamizi na Udhibiti wa kemikali.

“Kwenye banda la Mamlaka utapata taarifa zinazohusiana na madhara yanayotokana na kemikali za Viwandani na Majumbani pia kemikali za asili zinazotokana na uchimbaji wa madini mbalimbali, miamba mingi ina madini yanayoitwa silica kwa hiyo kwa kutokujikinga vizuri kunaweza kusababisha ugonjwa unaoshambulia mapafu unaojulikana kitaalamu kama silicosis, silicosis ikishaanza madhara yake ni makubwa kwa hiyo wananchi mpate elimu hii ili kujikinga na madhara ya kemikali  hizo za asili” Amesema.

Naye mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Mamlaka, Christine John Macha ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Noneria Products ametoa wito kwa wananchi wa Arusha na mikoa jirani kuweza kufika banda la Mamlaka kupata elimu ambayo itawasaidia katika shughuli zao za kila siku zinazotokana na kuwa kwenye maeneo yanayoweza kuwa na kemikali asili.

“Nitoe wito kwa wananchi wenzangu wa Mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani kufika katika banda hili la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kupata elimu ambayo itawasaidia katika kujikinga na madhara ya kemikali asili ambayo wengi wetu tumekuwa tukiishi katika mazingira  hayo kutokana na shughuli zetu za kila siku. Mimi nimeelimika na kufaidika kwa kufika katika banda hili, nimepata elimu ambayo itanisaidia katika shughuli zangu za kila siku” alisema.

Maonesho ya 30 ya Kilimo na Sherehe za Nane nane Kanda ya Kaskazini yanaendelea Jijini Arusha, kwenye viwanja vya Themi, Njiro yakijumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, kilele kikiwa tarehe 08.08.2024 na yamebeba Kauli mbiu ya “Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi