Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Je Matumizi ya sampuli na taarifa za Vinasaba yanalindwa kisheria kisheria?

Teknolojia ya vinasaba vya Binadamu ni moja kati ya teknolojia zinazokuwa kwa kasi zaidi duniani,kwa kupitia matumizi ya vinasaba vya binadamu,teknolojia hii inaweza kutumika kuboresha ustawi wa maisha ya watu kwa namna mbalimbali.

Teknolojia hii ikitumika ipasavyo huweza kutumiwa katika uchunguzi wa magonjwa mbalimbali na tiba, pia huweza kutumika katika utambuzi wa binadamu,kubaini uhalali wa watoto kwa wazazi  na utambuzi viungo mbalimbali vya binadamu.

Vinasaba vya binadamu vimebeba taarifa nyingi na muhimu kuhusu binadamu, Kutokana na umuhimu huo Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009 ina lengo la  kudhibiti na kusimamia matumizi sahihi ya vinasaba vya binadamu.Sheria ya Vinasaba vya Binadamu imeweka utaratibu wa uchukuaji wa sampuli, kufungasha, usafirishaji , kuhifadhi,uchunguzi pamoja na kuteketezwa kwa sampuli baada ya kukamilika kwa uchunguzi