Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) inasajili nini?

 

  • Maabara za kemia zinazotumika viwandani na majumbani
  • Maabara za hospitali zinazofanya uchunguzi wa vinasaba vya binadamu
  • Waingizaji, watengenezaji, watumiaji, wasambazaji, watunzaji, wasafirishaji, wateketezaji na wasafirishaji wa kemikali nje ya nchi.
  • Kemikali kama zilivyoainishwa katika Majedwali namba 3, 6, 7 na 8 ya Sheria Na. 3 ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani ya mwaka 2003. Unaweza kuzitambua pia kemikali hizi kwa kutumia njia ya Harmonised Shipping Code (HS Code) zenye namba kuanzia 22.07 mpaka 40.05.