Ni wadau gani wa kemikali wanapaswa kusajiliwa na GCLA ?
ikitaka kusajili kemikali, maabara ya kemikali, mdau wa kemikali, maabara za sayansi jinai au maabara ya vinasaba vya binadamu nifanye nini?
Ukitaka kusajili kemikali, maabara ya kemikali au mdau wa kemikali utatakiwa kuingia kwenye mfumo wa e-Services unaopatikana katika tovuti ya GCLA. Katika Tovuti hiyo ingia halafu ingia Customer Chemicals Management Portal, kisha ingia User Manual ambapo utapata maelekezo ya hatua kwa hatua ya jinsi ya kuanza usajili.
Ukitaka usajili wa Maabara ya sayansi jinai na Vinasaba vya Binadamu utatakiwa kutembelea Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo karibu na wewe, ofisi hizo zipo katika kanda sita kama zinavyoonekana katika Our Contacts kwenye tovuti ya GCLA.