Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

GCLA YAPONGEZWA KWA KUTOA RIPOTI ZA UCHUNGUZI KWA WAKATI

Imewekwa: 01 Feb, 2024
GCLA YAPONGEZWA KWA KUTOA RIPOTI ZA UCHUNGUZI KWA WAKATI

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepongezwa kwa kuimarisha utoaji wa ripoti za uchunguzi wa kimaabara za mashauri mbalimbali kwa muda mfupi.

Pongezi hizo zimetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. David Ngunyale katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, Kanda ya Dar es Salaam ambapo amesema utoaji wa ripoti za uchunguzi wa vinasaba kwa sasa umeimarika tofauti na hapo zamani.

“Hongereni sana utoaji wa ripoti za uchunguzi wa vinasaba kwa sasa umeimarika sana, kwa sasa ripoti zinatoka mapema ukilinganisha na hapo zamani. ”alisema Jaji Ngunyale.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi, ameipongeza Mamlaka kwa utendaji kazi uliotukuka huku akiishukuru Mamlaka kwa ushiriki wake katika maadhimisho hayo kama wadau muhimu katika mnyororo wa haki.

“Hongereni sana kwa kazi nzuri na nzito mnayoitoa kwa jamii na tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu katika maadhimisho haya”alisema Jaji Maghembe.

Maadhimisho ya Wiki ya sheria yameanza rasmi Januari 24, 2024 na yanatarajiwa kuhitimishwa Februari 1, 2024.